1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

YANGON: Zaidi ya watu laki moja washiriki kwenye maandamano makubwa

24 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBMv

Zaidi ya watu laki moja wakiongozwa na watawa wa madhehebu ya Budha wameandamana katika mji mkuu wa Yangon nchini Myanmar zamani Burma kupinga utawala wa kijeshi.

Maandamano hayo dhidi ya utawala wa kijeshi yamo katika siku yake ya saba leo na ni makubwa kuwahi kutokea katika kiindi cha miongo miwili.

Upinzani mkali dhidi ya serikali ya kijeshi ulinanza mwezi mmoja uliopita tangu serikali hiyo ilipotangaza nyongeza ya bei ya mafuta.

Hadi sasa maandamano hayo yamekuwa yakitekelezwa kwa njia ya amani na viongozi wake wameahidi kuendelea kuandamana hadi utawala wa kijeshi utakapoanguka.

Lakini wasiwasi umeanza kujitokeza baada ya walinda usalama nchini Myanmar kuanzisha misako.

Kiongozi wa upinzani Soe Aung amabae anaishi uhamishoni amesema.