YANGON:Aung San Suu Kyi aamini serikali inataka maridhiano
9 Novemba 2007Kiongozi wa upinzani wa Myanmar anayetumikia kifungo cha ndani Aung San Suu Kyi anaamini kuwa uongozi wa kijeshi nchini humo una nia ya kutafuta maridhiano ya kitaifa.Kauli hiyo inatolewa baada ya mkutano kati ya Bi Aung San Suu Kyi na afisa mmoja wa serikali.Wanachama wanne wa chama chake cha National League For Democracy NLD walikutana naye pia kwa yapata saa moja katika nyumba moja ya wageni ya serikali.
Mazungumzo yao yalikita katika mapendekezo ya namna ya kuendeleza mazungumzo kati ya serikali na upinzani ili kufikia makubaliano.
Kauli hiyo ilitolewa saa chache baada ya mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa Ibrahim Gambari kukamilisha ziara yake ya siku sita ya kujaribu kuwaleta pamoja wawakilishi wa uongozi wa kijeshi wa Myanmar na Bi Aung San Suu Kyi.