1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

YANGON:Aung San Suu Kyi ataka kushirikiana na serikali ya Junta

9 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C78h

Kiongozi wa upinzani nchini Myanmar anayetumikia kifungo cha ndani Aung San Suu Kyi amekutana na afisa wa serikali hii leo na kueleza haja yake ya kutaka kushirikiana na uongozi.Kiongozi huyo aidha amekutana na viongozi wengine wa chama chake kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 3.Suu Kyi anatumikia kifungo cha ndani kwa miaka 12 sasa.

Kwa mujibu wa mwanadiplomasia kutoka eneo hilo ambaye hakutaka jina lake lifahamike kiongozi huyo wa upinzani alikutana mwezi jana na afisa wa ngazi za juu wa serikali aliyeteuliwa kuwa mpatanishi.Uongozi wa kijeshi wa Myanmar ulitangaza hapo jana kuwa ung San Suu Kyi anakubaliwa kukutana na maafisa wa chama chake cha National League for Democracy.Kauli hiyo ilitolewa saa chache baada ya mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa Ibrahim Gambari kukamilisha ziara yake ya siku sita ya kujaribu kuwaleta pamoja wawakilishi wa uongozi wa kijeshi wa Myanmar na Bi Aung San Suu Kyi.