1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

YANGON:Mwakilishi maalum wa UN amaliza ziara yake nchini Myanmar

2 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/CBKk

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, nchini Myanmar Ibrahim Gambari ameondoka nchini Myanmar baada ya kukutana na wakuu wa kijeshi wa nchi hiyo pamoja na kiongozi wa upinzani.

Mwakilishi huyo wa Umoja wa Mataifa alikutana na Generali Than katika mji mpya mkuu wa Naypyitaw, lakini hakuna taarifa zaidi zilizotolewa kuhusiana na kile walichoafikiana.

Gambari baadaye alikutana na kiongozi wa upinzani Aung San Suu Kyi mara mbili hatua ambayo wanadiplomasia wa Asia wanasema kuwa ni ishara ya mafanikio katika harakati zake hizo.

Taarifa zinasema kuwa takriban waandamanaji 200 waliuawa katika harakati za utawala huo wa kijeshi kuyazima, kinyume na taarifa za serikali ya kwamba waliyouawa ni kumi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Myanmar Nyan Win akihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York alisema kuwa majeshi ya usalama ya nchi hiyo yalichukua tahadhari wakati wa kuyazima maandamano hayo.