1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

YANGON:Utawala wa Myanmar wazidi kupingwa duniani

7 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Hr

Maelfu ya waandamanaji wameandamana katika miji mbali mbali barani Ulaya na Asia kuupinga utawala wa kijeshi nchini Myanmar baada ya utawala huo kutumia nguvu kuyavunja maandamano ya wanaharakati wa kuetetea demokrasia nchini humo.

Waandamanaji wakiwemo watawa wa kibudha waliandana huko Taipei na London wakibeba mabango yanayoonyesha kuwaunga mkono wanaharakati wa Myanmar.Waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown ameutolea mwito Umoja wa Ulaya kuweka vikwazo vikali dhidi ya utawala wa Myanmar.Awali Uingereza Marekani na Ufaransa zilitoa taarifa kwa baraza la usalama la Umoja wa mataifa zikitaka utawala huo wa kijeshi ukomeshe matumizi ya nguvu na kuwaachia huru wafungwa wote wa kisiasa.Mjumbe maalum wa Umoja wa mataifa Ibrahim Gambari ambaye alikwenda Myanmar na kukutana na viongozi wa nchi hiyo alisema aliona mwanya wa matumaini ya kuwepo uwezekano wa kufanyika mazungumzo kati ya utawala huo wa kijeshi na kiongozi wa upinzani Aung San Suu Kyi.