1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiMorocco

Tetemeko la ardhi lawauwa zaidi ya watu 1,000 Morocco

9 Septemba 2023

Serikali ya Morocco imesema, kufikia sasa zaidi ya watu 1,000 wamefariki dunia kutokana na tetemeko la ardhi lililoitikisa nchi hiyo Ijumaa usiku

https://p.dw.com/p/4W97e
Watu wasafisha eneo la tetemeko la ardhi mjini Marrakech nchini Morocco mnamo Septemba 9, 2023
majengo yalioharibiwa na tetemeko la ardhi nchini MoroccoPicha: Abdelhak Balhaki/Reuters

Viongozi mbalimbali wa dunia na wanadiplomasia wametoa salamu za rambirambi baada ya tetemeko hilo lisilo la kawaida lililoathiri zaidi mji wa kitalii wa Marrakech. Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis ameonesha kusikitishwa kwake na janga hilo kupitia barua yake iliyochapishwa na Vatican akisema kuwa, anawaombea watu wote waliopoteza maisha na wale waliojeruhiwa katika tukio hilo.

Viongozi waonesha mshikamano na Morocco

Baadhi ya viongozi wa mataifa waliotuma salamu zao za pole kufuatia tetemeko hilo ni pamoja na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, Rais wa Marekani Joe Biden, Vladmir Putin wa Urusi, Emmanuel Macron wa Ufaransa, Volodymyr Zelensky wa Ukraine na Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi.