JamiiAsia
Zaidi ya watu 140 wafa kwa radi, dhoruba Pakistan
30 Aprili 2024Matangazo
Pakistan imekumbwa na mafuriko makubwa, maporomoko ya ardhi na hali mbaya ya hewa iliyosababisha nyumba kadhaa kubomoka huku katika baadhi ya maeneo kukiwa na uharibifu mkubwa wa mazao.
Msemaji wa Idara ya Hali ya Hewa nchini humo, Zaheer Ahmad Babar, amesema taifa hilo limeshuhudia mvua yenye "ongezeko la asilimia 164" ikiwa ni juu ya viwango vya kawaida katika mwezi huu wa Aprili.
Mnamo mwaka 2022, theluthi moja ya Pakistan ilifunikwa na maji kufuatia mvua kubwa kuwahi kushuhudiwa zilizosababisha mamilioni ya watu kuhama makaazi yao.
Benki ya Dunia inakadiria kuwa taifa hilo lilipata hasara ya dola bilioni 30 kutokana na mvua hizo.