1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiKorea Kusini

Zaidi ya watu 30 wamefariki katika mafuriko Korea Kusini

16 Julai 2023

Idadi ya vifo vilivyotokana na mvua kubwa na mafuriko Korea ya Kusini imefikia zaidi ya watu 30.

https://p.dw.com/p/4Txul
Südkorea, Gyeongsang | Überschwemmungen durch Starkregen
Picha: South Korean National Fire Agency/Getty Images

Vyombo vya habari vya nchi humo vimeripoti kuwa, miili 8 ilipatikana asubuhi ya leo katika njia ya chini ya ardhi iliyofurika katika mji wa Osong.

Soma pia: Mvua kubwa na mafuriko yasababisha vifo vya watu 24 Korea Kusini

Mamlaka za Korea kusini zinaamini kuwa, idadi hiyo huenda ikaendelea kuongezeka. Mpaka sasa watu 10 hawajulikani walipo tangu zilipoanza kunyesha mvua hizo tangu mwishoni mwa wiki iliyopita na kusababisha maporomoko ya ardhi na kukatika kwa umeme katika baadhi ya sehemu nchini humo.

Zaidi ya wakaazi 7,000 walilazimika kuondolewa kwenye makazi yao na kupelekwa kwenye maeneo salama mbali na mafuriko. Mamlaka ya hali ya hewa imetangaza kuwa, mvua zitaendelea kunyesha kwa siku chache zijazo katika sehemu kubwa nchini humo.