1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zanzibar yaadhimisha miaka 60 ya Mapinduzi

12 Januari 2024

Zanzibar leo inaadhimisha miaka 60 ya Mapinduzi. Katika hotuba yake ya kuadhimisha siku hii aliyoitoa jana usiku, Rais wa Zanzibar Hussein Ali Mwinyi amesisitiza kuyaenzi Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar

https://p.dw.com/p/4bA4B
Zanzibar | Rais Dr Hussein Mwinyi
Rais wa Zanzibar Hussein Ali MwinyiPicha: Shisia Wasilwa/DW

Zanzibar leo inaadhimisha miaka 60 ya Mapinduzi. Katika hotuba yake ya kuadhimisha siku hii aliyoitoa jana usiku, Rais wa Zanzibar Hussein Ali Mwinyi amesisitiza kuyaenzi Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa kutunza na kulinda amani na mshikamano.

Rais Mwinyi amesema mafanikio yaliyopatikana miaka 60 tangu yatokee Mapinduzi ya mwaka 1964, yametokana na uongozi thabiti wa viongozi wa awamu zilizotangulia kwa ushirikiano na uzalendo kati yao na wananchi.

Soma pia: Zanzibar yaadhimisha miaka 54 ya mapinduzi

Kiongozi huyo wa visiwa vya Zanzibar ameahidi kuendelea kutekeleza miradi ya maendeleo na kuleta usawa kwa wananchi wote.

Mapinduzi ya Zanzibar yalifanyika Januari 12 mwaka 1964 ambapo chama cha Afro Shirazi kwa kushirikiana na wanachama wa Chama cha Umma waliiondoa madarakani serikali ya mseto wa vyama vya Wazalendo wa Zanzibar, ZNP, na Chama cha Watu wa Zanzibar na Pemba, ZPPP na kutangaza Jamhuri ya Watu wa Zanzibar badala ya serikali ya Kisultani.