1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: Zanzibar yaelekea uchaguzi mkuu wa tano

15 Septemba 2015

Tanzania iko katika hekeheka za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, ukiwa ni wa tano tangu mfumo wa vyama vingi kurejeshwa na Zanzibar inashuhudia tena mchuano mkali kati ya CCM na CUF.

https://p.dw.com/p/1GWlo
GMF Diskussion Maoni
Picha: DW

Katika maoni mbele ya meza duara, macho yameelekezwa visiwani Zanzibar kuelekea uchaguzi mkuu. Matarajio, ilani za vyama na masuala makuu yanayojadiliwa na wengi miongoni mwa raia. Mohammed Abdul-Rahman amewaalika Hamza Hassan Juma kutoka CCM, Enzi Twalibu, Ali Swaleh na mwanasheria Ali Awadh Said, aliekuwa mjumbe wa tume ya kukusanya maoni ya wananchi kuhusu katiba mpya.

Unaweza kusikiliza kipindi kwa kubonyeza alama kisikilizio hapo chini.