1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Zelensky afanya mazungumzo na mkuu wa NATO

22 Julai 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema amezungumza leo na katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg kuhusu kufungua mlango bahari wa Bahari Nyeusi.

https://p.dw.com/p/4UGiJ
Litauen Vilnius | NATO-Gipfeltreffen 2023 | Selenskyj spricht zur Presse
Picha: Ints Kalnins/REUTERS

Zelensky amesema wamejadili tathmini za hali ya sasa na hatari kwa usalama wa chakula baada ya kuvunjika kwa mkataba huo. Wamezungumzia pia hatua zinazohitaji kuchukuliwa ili kufungua njia hiyo ya kupitishia nafaka katika Bahari Nyeusi.

Soma pia: Zelensky azungumza na Erdogan kuhusu kufufua mkataba wa kusafirisha nafaka

Wakati hayo yakiendelea, wizara ya ulinzi ya Urusi imesema, mwandishi mmoja wa habari za vita wa shirika la habari la RIA la Urusi ameuwawa na wengine watatu wamejeruhiwa katika shambulio kusini mashariki mwa mji wa Zaporizhzhia. Wizara hiyo imesema, Ukraine ilifanya shambulio kwa kutumia mabomu ya mtawanyiko kuwalenga waandishi.

Naye Gavana wa Crimea anayeungwa mkono na Urusiamesema, shambulio la droni lililoelekezwa katika ghala la mabomu kwenye rasi hiyo lilizilazimu mamlaka ziwaondoe watu waliokuwa ndani ya umbali wa kilometa tano.