Zelensky aisihi Ulaya kutochoka kuisadia Ukraine
7 Juni 2024Zelensky amewaambia wanasiasa hao wa Ufaransa kwamba rais Vladmir Putin ni mtu anayeipinga Ulaya na hatoishia na Ukraine katika juhudi zake za kunyakuwa maeneo. Amesema hali ya sasa barani Ulaya inayosababishwa na Putin ni sawa na ile iliyoshuhudiwa miaka ya 1930 wakati Hitler alipokuwa akiwaandama majirani zake.
"Ni nchini Ukraine ndiko unakokutikana ufunguo wa amani wa bara zima la Ulaya, kwa sababu bila ya kuwa na udhibiti wa Ukraine, Urusi italazimika kuwa taifa la kawaida na sio utawala wa kikoloni unaotafuta mara zote maeneo mapya ya kuyanyakuwa barani Ulaya, Asia na Afrika.'' Alisema kwenye hotuba yake.
Soma pia:Marekani kupeleka Ukraine msaada mpya wa kijeshi wa dola mil. 225
Ameishukuru Ufaransa kwa ahadi yake ya kupeleka ndege za kivita nchini mwake kama juhudi za kuimarisha hatua za kuilinda anga ya nchi hiyo dhidi ya mashambulizi ya Urusi.
Zelensky pia amezitolea mwito nchi za Magharibi kuchukuwa hatua zaidi kufikia amani itakayozingatia haki.