1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky asema hakuna mazugumzo ya amani ya Urusi

25 Septemba 2024

Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine ametupilia mbali uwezekano wa mazungumzo ya amani na Urusi, na badala yake ametowa wito wa kile alichokiita "hatua ya kilimwengu" kuilazimisha Moscow kukubali amani.

https://p.dw.com/p/4l2zf
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa / Volodymyr Zelensky
Rais Volodymyr Zelensky akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa tarehe 24 Septemba 2024.Picha: The Yomiuri Shimbun/AP/picture alliance

Zelensky alisema Urusi ilazimishwe kufuata matakwa ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa juu ya haki na heshima ya mataifa mengine.

Akizungumza kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hapo jana, Zelensky alidai kuwa Rais Vladimir Putin wa Urusi anatenda uhalifu wa kimataifa na amevunja kanuni nyingi za kimataifa na kamwe hawezi kuacha mwenyewe.

Soma zaidi: Zelensky: Umakini wa Marekani utaharakisha mwisho wa vita

Zelensky, ambaye yuko New York kuhudhuria Hadhara Kuu ya Umoja wa Mataifa, alisema kwamba ni kutokana na sababu hiyo, ndiyo maana njia pekee iliyopo ni kumlazimisha Putin kuacha vita na kuondoka Ukraine.

Kwenye mkutano huo wa Baraza la Usalama, mawaziri kutoka nchi 14 wanachama walihudhuria, huku Urusi ikituma balozi wake wa ngazi za chini kwenye Umoja wa Mataifa.