1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zelensky asema usalama wa Bahari Nyeusi ni muhimu kwa amani

26 Julai 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, amesema mkutano ujao wa Jumuia ya Kujihami ya NATO unapaswa kuangazia usalama wa bandari za Ukraine na usafirishaji wa nafaka

https://p.dw.com/p/4UOaZ
Themenpaket | Getreidehandel Getreide-Deal Grain deal Ukraine Russland
Picha: Pool Philip Reynaers/belga/dpa/picture alliance

Katika hotuba yake ya kila usiku kwa njia ya video, Zelensky amesema ulimwengu unajua kwamba usalama wa bandari za Bahari Nyeusi ni muhimu kwa amani na utulivu katika soko la chakula duniani.

Usalama wa chakula ni kipaumbele muhimu kote ulimwenguni

Kwa mujibu wa Zelensky, usalama wa chakula ni kipaumbele muhimu kote ulimwenguni na sehemu ya mfumo wa amani wa Ukraine. Katika eneo la mapambano, meli ya kivita ya Urusi kwenye Bahari Nyeusi imefanikiwa kuzuia shambulizi la Ukraine.

Urusi yasema Ukraine ilijaribu kushambulia meli yake ya doria

Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema Ukraine ilijaribu kuishambulia meli ya doria ya Sergei Kotov, kwa kutumia boti mbili zisizo na nahodha. Meli ya Kotov iliziharibu boti hizo zilizokuwa umbali wa mita 1,000 na 800. Hakuna mtu aliyejeruhiwa katika shambulizi hilo.