Zelensky atia saini sheria ya ongezeko la pesa kwa jeshi
21 Septemba 2024Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesaini sheria mpya ya ongezeko la karibu dola bilioni 12 kwa matumizi ya jeshi la nchi hiyo ili kuongeza mapambano katika vita vyake na Urusi.
Pesa hizo zitakazotumika kuwalipa wanajeshi walioko katika mstari wa mbele kwenye uwanja wa mapambano kuanzia mwezi huu zitatokana na ufadhili, mikopo na ongezeko la ushuru wa tumbaku na mafuta.
Soma zaidi. Urusi yavikomboa vijiji viwili magharibi mwa Kursk
Ukraine imekuwa ikijilinda dhidi ya uvamizi wa Urusi kwa zaidi ya miaka miwili na nusu.Na inasema imepokea zaidi ya dola bilioni 98 za msaada wa kifedha kutoka nje ya nchi tangu vita vilipoanza mnamo Februari 2022.
Hivi leo, Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine,Andriy Sybiha, amesema inaonekana kwamba Urusi inajiandaa kuvishambulia vituo vya nishati vya Ukraine kabla ya kuanza kwa msimu wa baridi na kuwataka washirika wa Ukraine kuanzisha mpango wa kudumu wa ufuatiliaji kwenye vinu vya nyuklia nchini humo.