1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zelensky awaomba washirika wake silaha zaidi kuikabili Urusi

6 Septemba 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amehudhuria mkutano wa kundi la kimataifa linalomuunga mkono unaofanyika katika kambi ya kijeshi ya Marekani ya Ramstein iliyoko Ujerumani.

https://p.dw.com/p/4kM1j
Ujerumani Ramstein | Volodymyr Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akizungumza wakati wa mkutano wa Kundi la Mawasiliano la Ulinzi la Ukraine katika kambi ya anga ya Marekani huko Ramstein, kusini-magharibi mwa Ujerumani.Picha: Daniel Roland/AFP/Getty Images

Kwenye mkutano huo, Rais Zelensky amewataka washirika wake hao kuipatia Ukraine silaha zaidi ili kuwaondosha wanajeshi Urusi kwenye ardhi yao.

Rais huyo wa Ukraine amewataka washirika wake kupuuzia mbali kitisho cha Urusi, ambayo imeyaonya mataifa ya Magharibi kutokuvuuka kile inachokiita "mstari mwekundu" kwenye ushirikiano wao na Ukraine kwenye vita hivi.

Soma pia: Mashambulizi ya Urusi yauwa 7 Lviv 

Zelensky aidha amerudia tena ombi lake la Ukraine kuruhusiwa kutumia silaha za Magharibi kushambulia sio tu ndani ya Urusi bali pia maeneo yake yanayokaliwa na Urusi.

Baadaye Rais Zelensky anatazamiwa kwenda nchini Italia kuzungumza na Waziri Mkuu Giorgia Meloni na kuhudhuria kongamano la uchumi.