Zelensky awasilisha "mpango wake wa ushindi" bungeni
16 Oktoba 2024Akihutubia bunge Zelensky amesema mpango huo ni muhimu kwasababu unalenga kurudisha mapigano katika eneo la adui, ili watu wa Urusi waweze kuelewa asili ya vita na hatimaye kuiwekea shinikizo Kremlin. Kipengele kingine cha mpango huo ni kwa nchi jirani za Kiev kudungua ndege zisizo na rubani zaUrusi juu anga ya Ukraine kutoka katika maeneo yao.
Zelensky pia alipendekeza kuweka silaha kubwa zisizo za nyuklia nchini Ukraine ili kuzuia Urusi kutokana na uchokozi zaidi. Rais wa Ukraine hapo awali aliwasilisha mpango wake wa ushindi kwa washirika wake wa Marekani, Ujerumani na Ufaransa lakini haukuweka wazi mambo mustakabali wa mpango huo hadharani.
Aidha rais Zelensky alitoa wito wa vikwazo ilivyowekewa vya kutumia makombora ya masafa marefu ya iliyo nayo kutoka nchi za Magharibi, akisisitiza hoja mabayo amekuwa akiirai washirika wake kuruhusu kwa miezi kadhaa.
Soma pia: Marekani yaimwagia mabilioni Ukraine kuongeza nguvu uwanja wa vita
Zelensky amesema "Washirika wa Ukraine, ambao tayari tumewawasilishia mpango huu, wameukubali. Wamekuwa wasikivu. Timu zinazingatia maelezo kwa ajili ya msaada wa ufanisi. Kesho, nitawasilisha Mpango wa Ushindi katika mkutano wa Umoja wa Ulaya ."
Muda wa kusitisha vita
Kansela wa UjerumaniOlaf Scholz amesema Berlin inatafuta njia za kumaliza mzozo wa Ukraine uliosababishwa na uvamizi wa Urusi, akisisitiza hatua hiyo lazima ifanyike kwa ushirikiano na Kyiv.
Katika hotuba yake kwa bunge la Ujerumani Scholz amesema "Pamoja na uungwaji mkono wa wazi kwa Ukraine, ni wakati wa sisi kufanya kila tuwezalo kubaini jinsi tunavyoweza kufikia hali ambayo vita hivi haviendelei kwa muda usiojulikana."
Mashambulizi yaendelea
Katika uwanja wa mapambano Urusi inadaiwa kufanya msururu wa mashambulizi makali ya droni ikilenga Kyiv na miji mingine na kusababisha moto kwenye kituo cha viwanda katika mkoa wa magharibi wa Ternopil. Kwa mujibu wa maafisa wa Ukraine vikosi vyake vya ulinzi wa anga vilidungua ndege zisizo na rubani 68 kati ya 136.
Soma pia: Ukraine yaimarisha ulinzi mashariki mwa Donetsk
Hata hivyo droni mbili zilirudi Urusi huku 64 hazijulikani zilipotua mara baada ya kunaswa na mifumo ya kielektroniki ya kivita na hakuna ripoti zozote za majeruhi.
/dpa,AFP