Zelensky kawaita Wajerumani marafiki wa kweli
14 Mei 2023Zelenskiy aliyewasili mjini Berlin usiku wa kuamkia leo Jumapili amefanikiwa kupata msaada mkubwa wa kijeshi, ambapo serikali ya Ujerumani ilitangaza kitita cha euro bilioni 2.7 siku ya Jumamosi, ukiwa msaada mkubwa kabisa tangu Urusi kuanzisha uvamizi wake mwezi Februari 2022.Akizungumza kwenye mkutano wa pamoja na waandishi wa habari akiwa na mwenyeji wake Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani, Zelenskiy amesema sasa ni wakati wa wao kuamua mwisho wa vita hivyo mwaka huu, na wananaweza kumfanya mvamizi kushindwa daima kwa mwaka huu.Kwa upande wake, Kansela Scholz alisisitiza ahadi ya Ujerumani kuendelea kuiunga mkono Ukraine kadiri itakavyohitajika, akipuuzia hali ya wasiwasi iliyokuwapo kabla kwenye mahusiano ya pande hizo mbili na kurukia suala jengine juu ya matarajio ya Kyiv kujiunga na Muungano wa Kijeshi wa NATO.