Ukraine yasema imeanza utengenezaji wa makombora
11 Aprili 2024Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema kuwa nchi hiyo imepiga hatua katika utengenezaji wa makombora ya ulinzi yatakayowezesha kupambana na Urusi.Zelensky: Wanajeshi 31,000 wa Ukraine wameuawa vitani
Katika ujumbe wake wa kila siku kwa njia ya vidio, Zelensky, alisema kuwa tayari wameanza kutengeneza aina mpya ya makombora, na ni muhimu sana kwa jeshi la nchi hiyo kuweza kuyatumia kupata mafanikio. Droni na makombora vinachukuliwa kuwa silaha muhimu zaidi katika vita.
Wakati huo huo, watu watatu wameuawa katikamashambulizi ya Urusi Kaskazini Mashariki mwa mkoa wa Kharkiv nchini Ukraine. Mkoa huo ulioko mpakani umekuwa ukilengwa kwa mashambulizi makali ya angani katika wiki za hivi karibuni.
Ripoti zinasema watu wengine wanne wamekufa na 14 wamejeruhiwa katika mashambulizi tofauti ya makombora ya Urusi kwenye mkoa wa bandari wa kusini wa Odessa.