Zelensky: Usambazaji wa silaha Ukraine umepungua
17 Novemba 2023Zelensky amewaambia waandishi wa habari kwamba silaha zinazopelekwa nchini humo zimepungua hasa makombora ya milimita 155 ambayo hutumiwa sana katika eneo la vita Mashariki na Kusini mwa nchi hiyo.
Urusi na Ukraine zimejizatiti kudumisha na kulinda hifadhi yao ya makombora baada ya takriban miaka miwili ya mapigano makali kati ya mataifa hayo mawili.
Korea Kusini yadai Pyongyang imeipelekea Urusi silaha
Korea Kusini imedai kuwa mshirika wa Urusi, Korea Kaskazini, imetuma mizinga milioni moja ili kuimarisha vita vya Urusi nchini Ukraine kwa kubadilishana na ushauri kuhusu teknolojia ya satelaiti.
Wakati huo huo Ujerumani imesema wiki hii kwamba Umoja wa Ulaya hautafikia lengo la mwaka mmoja la kupeleka makombora milioni moja nchini Ukraine, kwasababu Umoja huo unakabiliwa na changamoto katika kupata silaha hizo.