Zelensky atoa wito wa utekelezwaji wa mkataba wa nafaka
18 Julai 2023Zelensky amesema tayari amewaandikia barua rais wa uturuki Recep Tayyip Erdogan na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres juu ya kuendeleza mpango huo.
Zelensky asema makubaliano yanasalia kuwa halali
Zelensky amesema kuwa mpango wa usafirishaji nafaka katika Bahari Nyeusi unapaswa kuendelea hata bila ya Urusi na kwamba makubaliano ya usafirishaji nafaka ni kati ya Uturuki na Umoja wa Mataifa na yanasalia kuwa halali.
Urusi adai makubaliano hayatanufaisha mataifa maskini
Makubaliano hayo ya usafirishaji wa nafaka yaliruhusu tani milioni 32.9 za chakula kusafirishwa kutoka Ukraine tangu mwezi Agosti, na zaidi ya nusu yake zilielekea katzika mataifa yanayoendelea. Hata hivyo Urusi imedai kuwa mataifa maskini hasa ya Kiafrika hayakunufaika na makubaliano hayo.