Ziara ya rais wa Brazil Afrika inasaka ushawishi?
14 Februari 2024Kwa mujibu wa mwanadiplomasia huyo, nchi nyingi za bara Afrika zinarekodi viwango vya juu vya ukuaji wa Uchumi. Anasema umuhimu wao wa siasa za kikanda unaongezeka na ndio maana ni muhimu kwa Brazil kuimarisha mahusiano na Afrika.
Gelson Fonseca, ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Historia na Diplomasia (CHDD), ambayo hushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Brazili, anasema taifa lake lilikuwa na ushawishi Afrika hasa kuanzia miaka ya 70 na 80 katika nyanja ya huduma na biashara.
"Ni Dhahiri kulikuwa na kimya kwa sababu zinazojulikana na tukapoteza nafasi kiasi," alisema na kuongeza kuwa kutokana na maendeleo ya uwepo wa wengine na kutokana na kupungua kwa kasi ya makadirio barani Afrika, nafasi ya taifa hilo imezorota.
Rais Lula tayari alikuwa AngolaAgosti mwaka wa 2023. Ziara yake ya sasa itampeleka Misri na Ethiopia, ambako atahudhuria mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika – AU mjini Addis Ababa mnamo Februari 17 akiwa ndiye mgeni wa rasmi.
Nchi hizo mbili ni muhimu kimkakati kwa Brazil kwa sababu zimekuwa wanachama wa kundi la mataifa ya BRICS tangu mwanzoni mwa mwaka. Kundi hilo awali lilizijumuisha Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini.
Soma pia:Afrika Kusini na China zina maoni sawa kuitanua BRICS
Kisha likazifungulia mlango nchi kadhaa. Mauricio Santoro, ni mtalaamu wa masuala ya kimataifa katika Chuo Kikuu cha Rio de Janeiro, mtazamo wake unasema kuwa mataifa hayo mawili ya Afrika ni washirika muhimu wa kibiashara kwa Brazili.
"Misri ni muhimu sana katika uhusiano wa Brazil na Afrika. Kwa sasa ni mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Brazil katika bara la Afrika na Ethiopia ni nchi ambayo inapata umaarufu katika sera za nje za Brazil kutokana na kuingia kwake katikaBRICS." Alisema katika mahojiano
Hata hivyo, anatahadharisha dhidi ya kuwa na matumaini makubwa. Anasema kulikuwa na mapinduzi ya kijeshi nchini Misri na kuna vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Ethiopia.
"Kutokana na hali hii ya migogoro, matarajio ya kile Brazil inaweza kufikia hayapaswi kuwa ya juu sana." Alisisitiza
Mahusiano yanachochewa na mafungamano ya kihistoria
Brazil bado inaibua uhusiano chanya kwa watu wengi katika bara la Afrika, tofauti na Uingereza, Ufaransa na Ujerumani, nchi hiyo haichukuliwi kuwa dola la kikoloni.
Koloni hilo la zamani la Ureno ni nchi yenye watu weusi wengi zaidi nje ya Afrika na kwa pamoja na nchi nyingi za Kiafrika ina kumbukumbu za kutisha za utumwa uliofanywa na Ureno.
Nchi hiyo ambayo sasa ni ya tisa kwa nguvu ya kiuchumi duniani inachukuliwa kuwa mfano wa kuigwa katika nyanja nyingi za kiuchumi na kijamii.
Katika mkutano ujao wa kilele wa Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa kuanzia Februari 17 hadi 18, Rais wa Brazil Luiz Inácio Lula da Silva anaweza kuwa na uhakika wa mapokezi mazuri.
Soma pia:Karandinga: Chimbuko la Itikadi Kali
Tofauti na China na Urusi, ambazo zimeendelea kupanua uhusiano wao katika eneo hilo katika miaka kumi iliyopita, umuhimu wa kiuchumi wa Brazil umepungua. Biashara ya nje barani humo ilipungua kutoka dola bilioni 28 hadi dola bilioni 21 kati ya 2013 na 2023.
Kuna sababu nyingi za Brazil kujiweka mbali na Afrika. Ni pamoja na migogoro inayoendelea nchini mwake na athari za kashfa ya rushwa. Hii ilisababisha tuhuma za rushwa dhidi ya makampuni ya ujenzi ya Brazil.
Hii ilisababisha shutuma za ufisadi dhidi ya kampuni za ujenzi za Brazil ambazo zilidaiwa kujitajirisha katika miradi mikubwa katika nchi za Afrika. Rais wa zamani wa Brazil Jair Bolsonaro pia alionyesha kupendezwa kidogo na bara hilo.
Afrika kwenye ajenda ya G20
Lula anataka kuanzisha mabadiliko katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa. Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya ni wanachama wa kundi la G20, ambalo linazileta pamoja nchi muhimu zaidi zilizoendelea kiviwanda na zinazoibukia. Brazil inashikilia urais mwaka huu.
Soma pia:
Wakati wa urais wake wa G20, Brazil itahakikisha kwamba "maswala ambayo ni kwa maslahi ya Afrika yanawekwa kwenye ajenda ya G20". Moja ya masuala haya ni mapambano ya kimataifa dhidi ya njaa na umaskini.
Brazil imepata mafanikio makubwa katika uwanja huu. Mipango ya kijamii iliyozinduliwa katika miaka ya 1990 na kuimarishwa wakati wa mihula miwili ya kwanza ya Lula madarakani (2003 hadi 2010) imetoa mchango mkubwa katika kupunguza umaskini nchini humo.