1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ziara ya wafanya biashara wa Kijerumani Tanzania

5 Desemba 2008

Wawekezaji wa Kijerumani ziarani Tanzania

https://p.dw.com/p/G9Pk
Picha ya mji wa Dar es Salaam,TanzaniaPicha: DW /Maya Dreyer

Ujumbe wa wafanya biashara wa Kijerumani wanaoendesha shughuli zao Afrika, kupitia jumuiya yao ilioko mjini Hamburg , Afrika Verein, umekuweko Tanzania tangu Novemba 30 hadi jana, ukifanya mazungumzo na wenziwao pamoja na maafisa wa serekali ya Tanzania juu ya uwezekano wa kuwekeza katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki. Wafadhili wameisifu Tanzania, chini ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete, kutokana na utuilivu wake wa kisiasa, na mwaka jana uchumi wa nchi hiyo ulipanda kwa asilimia 6.6. Pia Umoja wa Ulaya umeihaidi nchi hiyo kuipatia misaada ya bajeti ya gharama ya Euro milioni 555 hadi mwaka 2013, misaada hiyo ikitiririka katika biashara, usafiri na kilimo.

Othman Miraji alizungumza kwa njia ya simu na Bibi Asmau Nitardy, afisa wa Jumuiya ya Afrika Verein , ambaye alifuatana na ujumbe huo huko Dar es Salaam. Kuhusu tathmini ya ziara hiyo.