Mahakama: Zuma hastahili kugombea uchaguzi wa Mei
20 Mei 2024Uamuzi huo umekuwa ukifuatiliwa kwa karibu kufuatia uwezekano wa kuathiri matokeo ya uchaguzi.
Kesi hiyo imetokana na uamuzi wa mwezi Machi wa Tume ya uchaguzi kumuondowa Zuma katika uchaguzi huo kwa madai kwamba katiba inakataza mtu yoyte aliyetumikia kifungo cha miezi 12 au zaidi kushikilia nafasi ya bunge.
Mwaka 2021 Zuma alifungwa miaka 15 jela kwa kushindwa kufika mahakamani kusikiliza kesi dhidi yake kwa tuhuma za kuhusika na rushwa.
Soma pia:Zuma azindua ilani ya uchaguzi kwa kutoa ahadi lukuki
Mwezi Aprili mahakama ikabatilisha uamuzi wake ikisema kipengee hicho cha katiba kinatumika kwa watu walio na nafasi ya kukata rufaa dhidi ya kesi zao na Zuma hakuwa katika kundi hilo.
Baadae tume ya uchaguzi ikapeleka kesi hiyo katika mahakama ya kikatiba.