Afrika Kusini yauondowa ujumbe wake nchini Israel
6 Novemba 2023Serikali ya Afrika Kusini imewaita nyumbani balozi wake na ujumbe wake wa kidiplomasia kutoka Israel, katika hatua ya kulaani mashambulizi yanayofanywa na nchi hiyo dhidi ya Ukanda wa Gaza.
Afrika Kusini imeyaita mashambulio hayo kuwa mauaji ya halaiki. Serikali ya Afrika Kusini piaimetishia kuchukuwa hatua dhidi ya balozi wa Israelnchini mwake kufuatia matamshi aliyoyatowa hivi karibuni kuhusu msimamo wa nchi hiyo ya Afrika katika vita kati ya Israel na Hamas.
Soma pia:Wapalestina zaidi ya 10 wauwawa kwa shambulio la Israel
Hakuna ufafanuzi zaidi uliotolewa kuhusu matamshi ya balozi huyo wa Israel.
Waziri wa Afrika Kusini katika ofisi ya rais Khumbudzo Ntshavheni Afrika Kusini imeamuwa kuwaita nyumbani wanadiplomasia wake wote kutoka Tel Aviv kwaajili ya mashauriano.
Waziri wa mambo ya nje Naledi Pandor ambaye leo amemkaribisha mwenzake wa Ukraine Dmytro Kuleba,amesema wanahitaji kushauriana na wanadiplomasia hao waliokuwa Tel Aviv kutokana na hali ya mauaji ya watoto inayowatia wasiwasi katika Ukanda wa Gaza.