Aliyepanga mapinduzi Sierra Leone akamatwa
6 Desemba 2023Mtu huyo ametajwa kuwa ni Amadu Koita, mwanajeshi wa zamani na mlinzi wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Ernest Bai Koroma.
Waziri wa habari wa Sierra Leone, Chernor Bah, amesema Koita aliyekuwa kati ya washukiwa wakuu waliokuwa wanatafutwa alikamatwa Jumatatu (Disemba 4).
Soma zaidi: Sierra Leone: Shambulio la Jumapili ni jaribio la mapinduzi
Watu 20 waliuwawa shambulizi la Jumapili nchini Sierra Leone
Kabla ya kukamatwa, Koita alihifadhiwa na polisi wawili ambao nao wamekamatwa.
Kukamatwa kwa Koita kunaifanya idadi ya watu wote wanaoshikiliwa kwa kuhusika na matukio ya jaribio hilo la mapinduzi kufikia 60, wengi wao wakiwa ni maafisa wa jeshi.
Mapema Novemba 26, washambuliaji wenye silaha walivamia maghala ya jeshi, kambi mbili, magereza na vituo viwili vya polisi na kupambana na vikosi vya usalama.
Katika tukio hilo watu 21 waliuwawa, wakiwemo wanajeshi 14.