1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sierra Leone: Shambulio la Jumapili ni jaribio la mapinduzi

28 Novemba 2023

Waziri wa habari aeleza kuwa shambulio la Jumapili lilikuwa jaribio la kuipindua serikali Sierra Leone.

https://p.dw.com/p/4ZY0K
Usalama | Wanajeshi wa Sierra Leone wakiwa katika doria
Wanajeshi wa Sierra Leone wakiwa katika doriaPicha: Issouf Sanogo/AFP

Waziri wa habari na mawasiliano wa Sierra Leone Chernor Bah amesema kuwa, mashambulizi kadhaa katika mji mkuu Freetown ikiwemo katika kambi ya kijeshi karibu na Ikulu ya raismnamo siku ya Jumapili yalikuwa ni jaribio lililoshindwa la kuipindua serikali.

Bah ameuambia mkutano na waandishi wa habari kuwa maafisa 13 wa kijeshi na rais mmoja wamekamatwa kwa kuhusika na jaribio hilo la mapinduzi.

Soma pia:Watu 20 waliuwawa shambulizi la Jumapili nchini Sierra Leone

Jana Jumatatu, rais Julius Maada Bio alipokea ujumbe kutoka jumuiya ya kiuchumi ya mataifa ya Afrika Magharibi ECOWAS ambayo Sierra Leone ni mwanachama uliosema wamefanya ziara ili kufikisha ujumbe wa mshikamano kutoka jumuiya hiyo.