1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaArgentina

Argentina imekataa rasmi uanachama wa BRICS

30 Desemba 2023

Argentina imekataa rasmi uanachama wa kundi la mataifa yanayoinukia kiuchumi BRICS. Rais wa nchi hiyo Javier Milei ametekeleza ahadi yake ya uchaguzi ya kubatilisha uamuzi wa nchi hiyo kujiunga na kundi hilo

https://p.dw.com/p/4aih2
Viongozi wa mataifa wanachama wa kundi la mataifa yanayoinukia kiuchumi  BRICS katika picha ya pamoja wakati wa mkutano wa kilele wa BRICS nchini Afrika Kusini mnamo Agosti 23, 2023
Viongozi wa mataifa wanachama wa kundi la mataifa yanayoinukia kiuchumi BRICSPicha: GIANLUIGI GUERCIA/AFP

Rais Milei ametuma barua kwa viongozi wa BRICS kurasimisha uamuzi wake wa kuiondoa nchi yake katika mpango wa kujiunga na kundi hilo la BRICS. Haya yametangazwa siku ya Ijumaa.

Rais Milei amesema kuwa wakati wa sasa sio ''fursa nzuri '' kwa Argentina kujiunga kama mwanachama kamili.

Soma pia:BRICS yakubali wanachama wapya sita

Mnamo mwezi Agosti, kundi hilo linalojumuisha mataifa ya G20 Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini, lilitangaza kuwapokea wanachama sita wapya.

Uanachama wa mataifa hayo sita yanayozijumuisha Argentina, Ethiopia, Iran, Saudi Arabia, Misri na Umoja wa Falme za Kiarabu ulipaswa kuanza kutekelezwa kuanzia Januari 1, 2024.