SiasaAsia
Azerbaijan na Armenia kusitisha mapigano ya Nagorno-Karabakh
20 Septemba 2023Matangazo
Vyombo vya habari vya Armenia vimeripoti hii leo juu ya kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano na Arzebaijan, yaliyodumu kwa siku mbili baada ya Arzebaijan kuanzisha operesheni ya kijeshi dhidi vikosi vya jimbo lililojitenga la Nagorno-Karabakh.
Ripoti hizo zimesema makubaliano hayo yametangazwa na mamlaka za jimbo hilo nchini Arzebaijan na yataanza kutekelezwa majira ya saa saba mchana ya eneo hilo hii leo.
Chini ya mkataba huo, vikosi vya Armenia vimetakiwa kuondoka Nagorno-Karabakh pamoja kuvipokonya silaha vikosi vya ulinzi kwenye eneo hilo.
Kulingana na Armenia mapema leo, karibu watu 32 wameuawa na wengine wengi wamejeruhiwa licha ya miito ya Urusi na Marekani ya kusitisha mapigano.
Soma pia: