Bayern washindi wa "Der Klassiker"
5 Desemba 2021Robert Lewandowski alifunga bao la ushindi, la pili katika mechi hiyo kupitia mkwaju wa penalti baada ya mwamuzi Felix Zwayer na msaidizi wa video (VAR) kuamua kuwa mpira uliomgonga mkono mchezaji wa Dortmund Mats Hummels kwenye eneo la hatari kuwa ulikuwa makusudi. Soma Bayern yaionyesha Dortmund nani mfalme wa Der Klassiker
Uamuzi huo ulimfanya kocha mkuu wa Dortmund, Marco Rose kutimuliwa uwanjani kutokana na hasira yake, baada ya kutazama timu yake ikicheza na Bayern kwa dakika 80 katika mchezo wa kusisimua, wenye ushindani mkali , lakini makosa ulitia dosari mechi hiyo.
soma Lewandowski mchezaji bora Ujerumani
Hummels hata hivyo alikuwa na bahati mbaya katika mechi hii kwani alihusika kwa njia moja ama nyengine katika mabao yote matatu ya Bayern.
Kipindi cha pili
Muda mfupi baada ya mchezaji Julian Brandt kuifungia Dortmund bao la mapema, Hummels alipoteza mpira katikati mwa duara alipobanwa na Thomas Müller, Bayern wakaitumia fursa na mshambuliaji Robert Lewandowski hakufanya makosa kusawazisha.
Muda mfupi kabla ya mapumziko, Raphael Guerreiro alipiga shuti lake moja kwa moja kwa Hummels na mpira ukampita na kumuendea Leroy Sané ambaye shuti lake lilitikisa wavu na kuiweka kifua mbele Bayern.
Nyota wa Dortmund Erling Haaland aliisawazishia Dortmund baada ya kipindi cha mapumziko, baada ya beki wa Bayern Dayot Upamecano kujaribu kila namna kudhibiti safu ya ulinzi.
Kipindi cha pili kiliendelea kwa kasi ile ile ya kufurahisha na hatimae Bayern iliangukia penalti na mchezaji Robert Lewandoski kunako dakika ya 77 ya mchezo akapa ushindi wa 3-2 Bayern Munich.
Hii ni mara ya sita mfululizo kwa Bayern kushinda mechi dhidi ya Dortmund maarufu kama "Klassiker" na kushindwa mara mbili kati ya mechi jumla 11 zilizopita za pambano hilo.
https://p.dw.com/p/43m7L