1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden kukutana na Zelensky

11 Julai 2023

Rais Joe Biden wa Marekani atakutana kwa mazungumzo na mwenzake wa Ukraine, Volodymyr Zelenskiy, kandoni mwa mkutano wa muungano wa kijeshi wa NATO katika mji mkuu wa Lithuania, Vilnus.

https://p.dw.com/p/4TiKw
Volodymyr Zelensky in Bulgarien
Picha: Georgi Paleykov/NurPhoto/picture alliance

Viongozi wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO wamekusanyika katika mkutano wa kilele ambao utatawaliwa na ajenda ya vita nchini Ukraine pamoja na shinikizo la Kyiv la kutaka ikaribishwe haraka ndani ya jumuiya hiyo.

Soma zaidi: Erdogan aondoa pingamizi kwa Sweden kujiunga na NATO

Nchi wanachama wa NATO wanajadili jinsi ya kuondokana na mgawanyiko kuhusu jitihada za Ukraine kutaka uanachama huo, lakini wanadiplomasia kadhaa wamebainisha kuwa tofauti hizo zimepungua baada ya walio wengi kuafiki kuwa Ukraine haiwezi kujiunga na NATO wakati huu wa vita.

Soma zaidi: Biden awasili Uingereza kabla ya mkutano wa NATO

Wanachama wa NATO katika Ulaya Mashariki wanaunga mkono msimamo wa Kyiv, wakihoji kwamba kuijumuisha Ukraine chini ya mwamvuli wa usalama wa pamoja wa muungano huo wa kijeshi unaoongozwa na mataifa ya Magharibi ndio njia bora ya kuzuia Urusi kuishambulia tena.