1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Blinken awasili Israel wakati vita vikiendelea huko Gaza

3 Novemba 2023

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amewasili Israel ili kushinikiza kuwasilishwa kwa misaada zaidi ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4YM41
Blinken anatarajiwa kutoa wito kwa Tel-Aviv kuheshimu sheria za kimataifa katika vita vyake huko Gaza.
Blinken anatarajiwa kutoa wito kwa Tel-Aviv kuheshimu sheria za kimataifa katika vita vyake huko Gaza.Picha: Jonathan Ernst/AP/picture alliance

Hii ni safari ya tatu ya Blinken huko Israel tangu kuanza kwa mzozo huu Oktoba 7 na anatarajiwa kutoa wito kwa Tel-Aviv kuheshimu sheria za kimataifa katika vita vyake huko Gaza.

Ijumaa hii pia, Kingozi wa kundi la Hezbollah Sayyed Hassan Nasrallah anatarajiwa kuzungumza kwa mra ya kwanza tangu kuanza kwa mzozo wa Israel na Hamas.

Jeshi la Israel limetangaza usiku wa jana kuwa limeuzingira kikamilifu mji wa Gaza huku likiendeleza mashambulizi yake katika lengo la kulitokomeza kundi la Hamas ambalo liliua watu 1,400.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya huko Gaza, zaidi ya Wapalestina 9,000 wameuawa huku 3700 wakiwa ni watoto.