1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blinken kuzungumza na Macron juu ya Ukraine, Gaza

2 Aprili 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, atafanya mazungumzo na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa mjini Paris hivi leo juu ya vita vya Urusi nchini Ukraine na vya Israel kwenye Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4eL5L
Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa
Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa. Picha: Sebastien Nogier/AP/picture alliance

Ufaransa na Marekani wamekuwa mstari wa mbele kuipatia Ukraine msaada muhimu wa kijeshi lakini wamekuwa na misimamo inayokinzana linapokuja suala la mzozo wa Mashariki ya Kati.

Soma zaidi: Marais wa Marekani na Urusi kuzungumza kwa simu juu ya mgogoro wa Ukraine

Serikali mjini Paris inashinikiza usitishwaji kabisa wa vita katika Ukanda wa Gaza.

Baada ya Paris, Blinken ataelekea mjini Brussels nchini Ubelgiji atakaposhiriki mazungumzo ya mawaziri wa mambo ya nje wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO kabla ya mkutano wa kilele wa maadhimisho ya miaka 75 ya muungano huo yatakayofanyika mjini Washington mwezi Julai.