1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge la Ulaya lapitisha mageuzi ya sera ya wahamiaji

Sylvia Mwehozi
11 Aprili 2024

Bunge la Umoja wa Ulaya jana Jumatano lilipitisha mageuzi makubwa ya sera za waomba hifadhi ambazo zitaimarisha taratibu za mipakani na kulazimisha mataifa yote 27 ya umoja huo kugawana majukumu.

https://p.dw.com/p/4edpx
Bunge la Ulaya
Bunge la UlayaPicha: Geert Vanden Wijngaert/AP Photo/picture alliance

Bunge la Umoja wa Ulaya jana Jumatano lilipitisha mageuzi makubwa ya sera za waomba hifadhiambazo zitaimarisha taratibu za mipakani na kulazimisha mataifa yote 27 ya umoja huo kugawana majukumu.

Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amesifu mageuzi hayo, akisema yatalinda mipaka ya Ulaya na kuhakikisha ulinzi wa haki za msingi kwa wahamiaji.

Kiongozi huyo aliongeza kuwa Umoja wa Ulaya ndio unapaswa kuamua nani wa kuingia Ulaya na kwa mazingira gani lakini sio walanguzi na wasafirishaji haramu wa binadamu.

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na waziri wa uhamiaji wa Ugiriki, Dimitris Kairidis, wote wameitaja kura hiyo kuwa ya kihistoria. Hata hivyo Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban amekosoa mageuzi hayo akisisitiza kuwa kunahitajika mabadiliko ili kukomesha wimbi la wahamiaji.