Bunge la Mashariki mwa Libya laidhinisha gavana mpya
30 Septemba 2024Matangazo
Uteuzi huo ulioidhinishwa siku ya Jumatatu (Septemba 30) ni sehemu ya juhudi za kuumaliza mgogoro ambao umesababisha kupungua kwa pato la mafuta nchini humo.
Katika kikao kilichooneshwa moja moja kwenye televisheni, bunge hilo pia lilimuidhinisha Mari Muftah Rahil Barrasi kama naibu gavana wa Benki Kuu.
Soma zaidi: Umoja wa Mataifa wautanzua mgogoro wa benki kuu ya Libya
Majina hayo mawili yalipendekezwa katika mkutano wa hivi majuzi uliosimamiwa na Umoja wa Mataifa.
Gavana huyo mpya hapo awali alikuwa ni mkurugenzi wa benki kuu aliyesimamia uwekaji na udhibiti wa fedha.