1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uturuki lapigia kura ombi la Finnland kujiunga na NATO

30 Machi 2023

Uturuki inatarajiwa leo kuwa mwanachama wa mwisho wa Jumuiya ya kujihami ya NATO kuridhia uwanachama wa Finland katika muungano huo wa ulinzi unaoongozwa na Marekani kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4PUZt
Türkei | Erdogan im türkischen Parlament
Picha: DHA

Bunge la Uturuki linapiga kura mchana huu kuhusu ombi la nchi hiyo ya UIaya Kaskazini kuwa mwanachama wa 31 wa NATO.

Hii ni baada ya Rais Recep Tayyip Erdogan kuhitimisha miezi ya mazungumzo na kulibariki ombi la Finland mapema mwezi huu.

Uturuki yapanga kuidhinisha ombi la Finland kujiunga na NATO

Erdogan analidhibiti bunge kupitia muungano na chama cha siasa za mrengo wa kulia. Wabunge wengi wa upinzani pia wanaunga mkono ombi la Finland.

Idhini ya Uturuki itaiacha Finland,  ambayo inapakana na Urusi, na hatua chache tu za kiufundi kabla ya kujiunga rasmi na NATO.