Uturuki yapanga kuidhinisha ombi la Finland kujiunga na NATO
16 Machi 2023Matangazo
Taarifa hiyo imetolewa wakati Rais wa Finland Sauli Niinisto akitarajiwa hivi leo kufanya ziara nchini humo.
Sweden na Finland zilituma maombi mwaka jana kujiunga na NATO baada ya Urusi kuivamia Ukraine, lakini Sweden inakabiliwa na pingamizi kutoka Uturuki.
Finland yatumai kukubaliana na Uturuki kuhusu NATO
Ankara inasema Stockholm inawahifadhi wanachama wa vikundi vya kigaidi, jambo linalokanushwa na Sweden.
Mabunge ya nchi wanachama wote 30 wa NATO lazima yaidhinishe maombi ya uanachama kwa muungano huo. Mbali na Hungary, Uturuki ndiye mwanachama pekee ambaye bado hajaidhinisha maombi ya Finland na Sweden.