SiasaBurkina Faso
Burkina Faso na Urusi wajadiliana kuhusu ushirikiano
9 Oktoba 2024Matangazo
Wizara ya ulinzi ya Urusi ilisema jana kuwa nchi hiyo imekuwa ikifuatilia maslahi ya kijeshi, kidiplomasia na kiuchumi barani Afrika, ikishindana na nchi za Magharibi.
Burkina Faso, chini ya utawala wa kijeshi tangu mapinduzi ya 2022, imekuwa ikiwapokea wapiganaji mamluki wa kundi binafsi la kijeshi la Urusi, Wagner.
Mwezi Juni, Urusi ilisema itapeleka vifaa zaidi vya kijeshi na wakufunzi Burkina Faso, ili kuisaidia nchi hiyo kuimarisha uwezo wake wa kiulinzi na kupambana na ugaidi.
Katika mkutano wa kilele kati ya Urusi na Afrika, mwaka 2023, Putin alisema Urusi imesaini mikataba ya kijeshi na kiufundi na nchi 40 za Afrika, ambayo inaweza kufungua mlango wa mauzo zaidi ya silaha za Urusi kwenye eneo hilo.