1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BvB wahifadhi taji la Bundesliga

23 Aprili 2012

Rangi ya njano ilitanda kote mitaani Ujerumani huku mashabiki wa Borussia Dortmund wakisherekea ushindi wa taji la ligi ya soka Ujerumani - Bundesliga kwa mara ya pili mfululizo.

https://p.dw.com/p/14jkq
Fußball Bundesliga, 32. Spieltag, Borussia Dortmund - Borussia Mönchengladbach am Samstag (21.04.2012) im Signal-Iduna-Park in Dortmund. Die Dortmunder Mannschaft mit Mannschaftskapitän Sebastian Kehl (r) an der Spitze rutschen auf Knien über den Rasen. Dortmund gewinnt 2:0 und ist damit zum 8. Mal Deutscher Fußballmeister. Foto: Roland Weihrauch dpa/lnw
Fußball, Bundesliga 32. Spieltag, Borussia Dortmund Borussia Mönchengladbach MeisterfeierPicha: picture-alliance/dpa

Ushindi huo ulithibitisha kuibuka kwa Borusssia Dortmund kama hasimu mkuu wa klabu ya Bayern Munich katika soka ya ligi kuu Ujerumani Bundesliga.

Dortmund ilikuwa timu ya kwanza kando na Bayern, kuhifadhi taji la Bundesliga tangu ilipofanya hivyo miaka 16 iliyopita, na kumaliza desturi ya Bayern ya kushinda taji la ligi karibu kila msimu wa pili tangu mwaka wa 1996.

Dortmund ilinyakua taji lake la nane la ligi ya Ujerumani Jumamosi wakati ilipoendeleza rekodi ya Bundesliga ya kutoshindwa katika mechi 26 mfululizo. Kocha wa Dortmund Jurgen Klopp alisema uinshangaza kuona wanachofanya.

Mashabiki wa Dortmund walisherekea Borussia shindi wao kote mitaani, Ujerumani
Mashabiki wa Borussia Dortmund walisherekea ushindi wao kote mitaani UjerumaniPicha: picture-alliance/dpa

Ikiwa watashinda michuano yao iliyosalia, Dortmund itaweka rekodi ya Bundesliga ya kumaliza ligi na alama 81, wakati pia ikiwa na nafasi ya kunyakua taji jingine la nyumbani la Kombe la Shirikisho, mnamo tarehe 12 mwezi ujao wa Mei dhidi ya Bayern. Bayern Munich nao pia walishinda mchuano wao dhidi ya Werder Bremen magoli mawili kwa moja.

United na City kukutana ana kwa ana

Katika ligi kuu ya soka Uingereza ilichukua mkondo mwingine ambao haukutarajiwa jana jumapili wakati Manchester City ilipowazaba Wolverhampton magoli mawili na kupunguza hadi pointi mbili pengo baina yao na Manchester United waliotoka sare ya magoli manne na Everton.

Huku mahasimu hao wawili wakijiandaa kukutana ana kwa ana uwanjani Etihad katima mchuano wa marudiano nao Ctiy wakiwa na faida kubwa ya magoli kuliko United, hatima ya taji hilo imerejea tena mikononi mwao wote katika kile kinachoonekana kuwa kilele cha msimu huu. Mkufunzi wa United Sir Alex Ferguson aliwafokea wachezaji wake kwa kuzembea

Man United itakuwa mgeni wa Man City tarehe 30.04.2012
Man United itakuwa mgeni wa Man City tarehe 30.04.2012Picha: dapd/DW-Montage

Ferguson anasema huo ndio utakaokuwa mchuano mkali zaidi maishani mwake kuwahi kuhushudia tangu alipochukua usukani wa Manchester United mwaka wa 1986. Lakini Kocha wa Man City Roberto Mancini amesema bnado United wana nafasi kubwa ya ushindi. Mlinda lango wa City Joe Hart anasema pambano lao dhidi ya United ndilo wanalolisubiri. Aliongeza kuwa wanahisi kuwa tayari na pia wanafunga magoli.

Katika mchuano mwingine wa jana Liverpool iliendelea matokeo duni baada ya kushindwa na Westbrom Albion goli moja kwa bila.

Ligi ya Mabingwa Ulaya

Chelsea wanajiandaa kwa kibaria kikali kesho Jumanne dhidi ya Barcelona wakati klabu hiyo ya Uhispania ikilenga kufufuka kutokana na fedheha ya ligi y anyumbani La Liga waliposhindwa magoli mawiki kwa moja na Real Madrid ambao wanakaribia kutwaa taji jilo.

Barcelona ina rekodi nzuri katika uwanja wa nyumbani Camp Nou
Barcelona ina rekodi nzuri katika uwanja wa nyumbani Camp NouPicha: Reuters

Barcelona wanalenga kushiriki katika fainali ya Champions League kwa mara ya tatu katika misimu mine. Mabingwa hao watetezi waliduwazwa goli moka kwa sifuri katika duru ya kwanza uwanjani Stamford Bridge. Kocha wa Barca Pep Guardiola ameonyesha matumaini kuwa vijana wake wamejiandaa vya kutosha kupambana na Chelsea uwanjani Camp Nou. Chelsea bila shaka wanafahamu kuwa walikuwa na kibarua kigumu katika mkondo wa kwanza licha ya kuwa walisajili ushindi, na kaimu mkufunzi Roberto Di Matteo anasema utakuwa mchezo mgumu, kiakili na kimwili pamoja na shinikizo kubwa.

Siku ya Jumatano, itakuwa zamu ya Bayern Munich kusafiri uwanjani Santiago Bernabeu nchini Uhispania kupambana na real Madrid. Bayern wanasafiri wakifahamu kazi walio nayo wakati wakilenga kufuzu katika fainali ambayo itachezwa katika uga wao wa nyumbani Allianz Arena. Katika mkondo wa kwanza Bayern iliwafunga Real magoli mawili kwa moja.

Mwandishi: Bruce Amani/Reuters/AP

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman