Chadema kuwachagua viongozi wa juu
21 Januari 2025Matangazo
Mwenyekiti anayemaliza muda wake Freeman Mbowe, na Tundu Lissu ambaye ni Makamu Mwenyekiti-Tanzania bara wamesema hii leo kwamba ni muhimu kwao kuendeleza mshikamano na kukijenga chama, bila kujali nani atachaguliwa kuwa mwenyekiti mpya.
Chadema yakamilisha hatua ya kwanza ya uchaguzi wa mabaraza
Akizungumza na wajumbe wa mkutano wa chama hicho unaofanyika katika jiji la kibiashara la Dar es salaam, Mbowe amesisitiza umuhimu wa umoja na nidhamu ndani ya Chadema, akitoa rai kwa wanachama kujizuia na matusi na migogoro ya ndani.
Kwa upande wake Lissu, ameahidi kujitolea kwake katika kukiimarisha chama bila kujali matokeo ya uchaguzi huo wa uongozi.