SiasaAfrika Kusini
Chama tawala cha Afrika Kusini chaelekea kupoteza wingi
31 Mei 2024Matangazo
Kwa mara ya kwanza tangu chama cha ANC kiingie madarakani miaka 30 iliyopita, huenda kikapungukiwa na viti vya kukiwezesha kulidhibiti bunge na hivyo kulazimika kuingia katika serikali ya mseto.
Chama kikuu cha upinzani cha Democratic Alliance mpaka sasa kimefikia asilimia 23.7 huku chama cha uMkhoto weSizwe cha rais wa zamani, Jacob Zuma kikiwa na asilimia 10.8, na kile cha wapigania ukombozi wa kiuchumi, EFF cha Julius Malema kikifikia asilimia 9.6 ya kura.
Matokeo kamili yanatarajiwa kufahamika mwishoni mwa wiki.