Chama tawala nchini Japan kumchagua kiongozi mpya
27 Septemba 2024Chama tawala nchini Japan cha Liberal Democratic Party (LDP), kitamchagua hivi leo kiongozi wake mpya ambaye pia atachukua nafasi ya waziri mkuu wa taifa hilo.
Wabunge tisa, wakiwemo wanawake wawili ndio wanaogombea nafasi hiyo lakini vigogo watatu wa chama hicho akiwemo waziri wa zamani wa ulinzi Shigeru Ishiba na Waziri wa Mazingira Shinjiro Koizumi, ndio wanaopewa kipaumbele.
Waziri Mkuu wa sasa Fumio Kishida,anayetarajiwa kujiuzulusiku ya Jumanne, anakabiliwa na kashfa za ufisadi na chama chake kinatafuta kiongozi mpya katika jitihada za jaribu kurejesha imani ya umma.
Mfululizo wa serikali za muda mfupi umekuwa ukitatiza uwezo wa mawaziri wakuu wa Japan kuwa na malengo ya muda mrefu kwenye sera zao au kuendeleza mahusiano ya kuaminika na viongozi wengine duniani.