1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chanjo 10,000 za Mpox zinatarajiwa kuwasili Afrika

Hawa Bihoga
25 Agosti 2024

Dozi elfu kumi za kwanza za chanjo ya Mpox zinatarajiwa kuwasili juma lijalo barani Afrika ambapo aina mpya ya virusi hatari vya ugonjwa huo uliosumbua kwa miongo kadhaa imesababisha wasiwasi wa kimataifa.

https://p.dw.com/p/4jtoe
Dozi za chanjo ya Mpox
Dozi za chanjo ya MpoxPicha: Gideon Markowicz/Xinhua News Agency/picture alliance

Hadi mwezi Agost Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa WHO, linatakiwa kuanza rsmi mchakato wa kuzirahisishia nchi masikini kupata kiwango kikubwa cha chanjo kupitia mashirika ya kimataifa.

Katika hatua nyingine Waziri wa Afya nchini Kongo- Brazzaville Gilbert Mokoki amesema visa ishirini na moja vya Mpox vimerekodiwa nchini humo.

Soma pia:WHO yatoa idhini kwa Gavi na Unicef kununua chanjo ya Mpox

Ameongeza kwamba nchi hiyo ya Afrika ya Kati imesajili visa 158 vinavyoshukiwa tangu mwanzoni mwa mwaka huu na 21 kati ya hivyo vimethibitishwa.

Visa vya ugonjwa huo wa kuambukiza ambao zamani ukijulikana kama MonkeyPox vimekuwa vikiongezeka katika eneo la mashariki na kati mwa Afrika, lakini virusi hivyo vimegundulika pia katika maeneo mengine ikiwemo barani Asia na Ulaya, huku Shirika la Afya duniani WHO likitangaza dharura ya kimataifa.