1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroChina

China yafanya luteka karibu na Bahari ya China Kusini

Saleh Mwanamilongo
28 Septemba 2024

Meli na ndege za China zimefanya doria kwenye eneo la Scarborough Shoal katika Bahari ya Kusini ya China, huku Beijing ikiendelea kudai umiliki wa takriban jumla ya eneo hilo.

https://p.dw.com/p/4lBv5
China yafanya luteka karibu na Bahari ya China Kusini inayozozaniwa
China yafanya luteka karibu na Bahari ya China Kusini inayozozaniwaPicha: Adrian Portugal/REUTERS

Doria hiyo inafanyika baada ya makabiliano makali na Ufilipino kwenye eneo la bahari lenye mzozo, katika miezi ya hivi karibuni.

Doria hiyo pia imeambatana na luteka ya pamoja iiliyofanywa na Marekani, Australia, Japan, New Zealand na Ufilipino katika eneo la kipekee la kiuchumi la Manila.

Hatua hiyo ya China imefanyika muda mfupi baada ya mazungumzo kati ya Waziri wa Mambo ya Nje Wang Yi na mwenzie wa Marekani Antony Blinken mjini New York kuhusu njia za kupunguza mivutano katika eneo hilo la Asia Kusini.