1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

China yakasirishwa makamu wa rais wa Taiwan kutua Marekani

12 Agosti 2023

Makamu wa Rais wa Taiwan William Lai aliye njiani kuelekea Paraguay anatarajiwa kusimama kwa muda nchini Marekani leo, uamuzi ambao umeighadhibisha China.

https://p.dw.com/p/4V5j2
Makamu wa Rais wa Taiwan William Lai
Makamu wa Rais wa Taiwan William LaiPicha: SAM YEH/AFP

Mara zote, China hukosoa safari za maafisa wa kisiwa hicho wanaopitia Marekani. Lai atasimama nchini Marekani mara mbili akiwa njiani kwenda na kutoka Paruguay anakotatarijiwa kuhudhuria dhifa ya kuapishwa rais mpya wa taifa hilo.

Hii leo atapitia mjini New York na wakati wa safari yake ya kurejea nyumbani atatua kwa muda mfupi mjini San Fransinco.

Soma zaidi: China yaituhumu Marekani kuigeuza Taiwan kuwa eneo hatari

China imekasirishwa na ratiba hiyo ya safari na imeitaka Washington kuheshimu sera ya China kwa kusitisha mahusiano na Taiwan, kisiwa ambacho Beijing inakizingatia kuwa sehemu ya himaya yake.

Mnamo mwezi April China ilijibu safari kama hiyo kwa kufanya luteka ya kijeshi baada ya rais Tsai Ing-wen wa Taiwan kusimama kwa muda huko California na kufanya mazungumzo na spika wa Baraza la Wawakilishi la Bunge la Marekani Kevin McCarthy