1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

China yapeleka ndege za kivita katika anga ya Taiwan

24 Mei 2024

China inafanya luteka ya kijeshi kwa mashambulizi ya makombora na kupeleka ndege za kivita ikiwa ni katika mazoezi yake ya siku mbili dhidi ya Taiwan.

https://p.dw.com/p/4gEgS
Taiwani | Ndege ya Jeshi la Anga la Taiwan F-16 ikiruka wakati wa safari ya doria
Taiwani | Ndege ya Jeshi la Anga la Taiwan F-16 inapaa wakati wa doria - Mei 24, 2024Picha: Taiwan Defence Ministry/Handout/REUTERS

Kwa mujibu wa televishini ya China CCTV, kwenye jaribio hilo ndege za mashambulizi na vikosi vya wana maji zilionekana zikifanya mashambulizi yasio halisi. Kadhalika zilionekana kupanga safu kijeshi kwa uelekeo wa maeneo kadhaa za mashambulizi katika upande wa bahari wa mashariki.

Luteka hiyo ya kijeshi inafanyika ikiwa ni takriban siku tatu tu baada ya rais mpya wa Taiwan Lai Ching-te kuanza kazi rasmi. Taiwan imelaani vitendo vya China.

China imekuwa ikikichukulia kisiwa cha Taiwan chenye kujitawala chenyewe kidemokrasia kama sehemu yake na kumshutumu Rais Lai kama mtu wa utengano. Inamkosoa vikali kufuatia hotuba yake ya mwanzo, ambayo aliitaka serikali ya Beijing kusitisha vitisho na kwamba pande zote mbili za ujia wa bahari hazina udhibiti wa upande wowote.

Jeshi lasema lengo ni kujipima uwezo wa udhibiti

China, Beijing | Kugubikwa kwa mazoezi ya kijeshi ya China karibu na Taiwan
Runinga kubwa huko Beijing inaonyesha jeshi la China likianza mazoezi ya siku mbili kuzunguka Taiwan Mei 23, 2024.Picha: Kyodo/picture alliance

Katika taarifa yake kamandi ya kijeshi ya jeshi la China kwa upande wa mashariki imesema mazoezi hayo yaliyopewa yaliyopewa jina la Upanga wa Pamoja - 2024A, yana shabaha ya kujaribu uwezo wa kunyakua madaraka kwa pamoja, kuanzisha mashambulizi ya pamoja na kuchukua maeneo muhimu.

Afisa mmoja mwandamizi katika masuala ya usalama wa Taiwanaliiambia Reuters kwamba washambuliaji wa China walifanya mashambulizi ya dhihaka dhidi ya meli za kigeni katika maeneo ya karibu mwishoni mwa mashariki wa Bashi Channel, sehemu ambayo inaitenganisha Taiwan kutokea Ufilipino, wakifanya mazoezi ya jinsi ya kukamata "udhibiti kamili" wa maeneo ya magharibi.

Afisa huyo, ambae alizungumza pasipo kutaka kufahaamika jina lake kutokana na unyeti wa hali, amesema boti kadhaa za walinzi wa pwani ya China pia wamefanya kile kilichoitwa mashambulio ya kuitishia Taiwan kwenye pwani ya mashariki ya kisiwa hicho, ikiwa ni pamoja na ukaguzi wa meli za raia.

Soma zaidi:Baraza la Seneti la Marekani laidhinisha msaada kwa Ukraine

Lakini kwa upande wao walinzi wa pwani wa China walisema kuwa wameendesha utekelezaji wa mazoezi wa sheria katika eneo la bahari la mashariki mwa Taiwan kwa siku ya leo, wakilenga mafunzo juu ya uthibitishaji na utambuzi na tahadhari.

Hata hivyo wachambuzi, wanadiplomasia wa kikanda na maafisa wakuu wa Taiwan wanasema kwa ulinganifu ukubwa wa mazoezi hayo hadi wakati huu, hayana uzito ukilinganisha mazoezi kama hayo ya 2022 ingawa wameonesha mashaka ya kutokea ajali katika utekelezwaji wake.

Chanzo: RTR