1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Dissanayaka kuapishwa rais wa Sri Lanka

23 Septemba 2024

Rais mteule anayefuata siasa za mrengo wa kushoto anatarajiwa kuapishwa leo nchini Sri Lanka, kufuatia ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi uliogubikwa na hasira za wapigakura dhidi ya hali ngumu ya uchumi.

https://p.dw.com/p/4kxRY
Anura Kumara Dissanayaka
Anura Kumara DissanayakaPicha: REUTERS

Anura Kumara Dissanayaka wa chama JVP amemtangulia mshindai wake wa karibu kwa zaidi ya kura milioni 1.3.

Kiongozi huyo aliyejitangaza kufuata siasa za Kimarx na ambaye chama chake kiliongoza maandamano ya umma mara mbili yaliyopelekea vifo vya maelfu ya raia, alipata uungaji mkono mkubwa kufuatia mporomoko wa uchumi wa mwaka 2022.

Soma zaidi: Dissanayaka atangazwa rais mteule katika uchaguzi wa Sri Lanka

Dissanayaka, mwenye umri wa miaka 55, anaapishwa asubuhi ya leo kumrithi Rais Ranil Wickremesinghe, mwenye umri wa miaka 75, ambaye alichukuwa madaraka kufuatia mapinduzi ya umma.

Wickremesinghe aliongoza kwa kuongeza kodi na hatua nyengine za kubana matumizi akifuata masharti ya Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF.

Ingawa alifanikiwa kuondosha upungufu wa huduma muhimu na kuurejesha uchumi kwenye hatua za ukuwaji, lakini aliwasababisha mamilioni ya raia kuingia kwenye ufukara mkubwa zaidi.