1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Droni za Ukraine zashambulia kituo cha mafuta Rostov, Urusi

18 Agosti 2024

Droni za Ukraine zimekishambulia kituo cha kuhifadhi mafuta katika eneo la Rostov kusini mwa Urusi mapema hii leo na kuzua moto mkubwa wa mafuta, hayo yamesemwa na gavana wa eneo hilo.

https://p.dw.com/p/4jb8C
Urusi
Droni za Ukraine zimekishambulia kituo cha kuhifadhi mafuta katika eneo la Rostov kusini mwa Urusi mapema hii leo na kusabibsha moto mkubwaPicha: Russia Emergency Ministry/dpa/picture alliance

Droni za Ukraine zimekishambulia kituo cha kuhifadhi mafuta katika eneo la Rostov kusini mwa Urusi mapema hii leo na kuzua moto mkubwa wa mafuta, hayo yamesemwa na gavana wa eneo hilo.

Video zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii zilionesha moshi mzito mweusi na miale ya moto ikitoka kwenye eneo hilo. Gavana huyo alisema kupitia mtandao wa Telegram kwamba moto huo ulikuwa katika mji wa Proletarsk.

Soma zaidi. Ukraine yasema inaimarisha nafasi ya vikosi vyake, Urusi

Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema ilizidunguwa droni tano za Ukraine usiku wa kuamkia leo, zikiwemo mbili katika eneo la Rostov .

Ukraine imevilenga mara kwa mara vituo vya mafuta na gesi nchini Urusi vilivyopo jirani na mipaka yake tangu mzozo huo ulipoanza mwaka 2022, ikidai kuwa inalipiza kisasi kwa mashambulizi kama hayo ya Urusi dhidi ya miundombinu yake ya nishati.