1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiEthiopia

Ethiopia kufungua soko la hisa ili kuwavutia wawekezaji

Saleh Mwanamilongo
11 Januari 2025

Ethiopia haijawahi kuwa na soko la hisa kwa miaka 50, tangu kuanguka kwa Mfalme Haile Selassie mwaka wa 1974 ambaye alitaifisha uchumi.

https://p.dw.com/p/4p3iX
Kampuni zingine ikiwa ni pamoja na benki na kampuni za bima, zinatarajiwa kusajiliwa baadae
Kampuni zingine ikiwa ni pamoja na benki na kampuni za bima, zinatarajiwa kusajiliwa baadaePicha: Solomon Muchie/DW

Ethiopia imezindua soko lake la hisa, ikiwa ni hatua ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed ya kuokoa uchumi wa nchi hiyo unaosuasua. Kampuni ya kwanza kuorodheshwa kwenye soko hilo ni Ethio Telecom, kampuni ya simu inayomilikiwa na serikali. Kampuni zingine ikiwa ni pamoja na benki na kampuni za bima, zinatarajiwa kujisajiliwa baadae.

Serikali ilipanga mauzo ya kwanza ya hisa katika Ethio Telecom mwezi Oktoba, kuruhusu hadi asilimia 10 ya hisa kuuzwa. Katika miezi ya hivi karibuni, mamlaka imepitisha mfululizo wa mageuzi ya kiuchumi ili kuvutia wawekezaji.

Ethiopia haijawahi kuwa na soko la hisa kwa miaka 50, tangu kuanguka kwa Mfalme Haile Selassie mwaka wa 1974 ambaye alitaifisha uchumi.