1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Human Rights Watch yasema dhulma zaendelea Tigray Magharibi

1 Juni 2023

Huma Rights Watch imezishutumu mamlaka za ndani na vikosi vya jimbo la Amhara kuendelea kuwafukuza kwa lazima Watigranya, kama sehemu ya kampeni ya takasa takasa ya kikabila magharibi mwa Tigray licha ya mapatano.

https://p.dw.com/p/4S3HE
Äthiopien Mekelle | Tigray-Streitkräfte  Übergabe von  Waffen an äthiopische Armee
Picha: Million Hailessilasie/DW

Human Rights Watch imesema katika ripoti yake iliyochapishwa hii leo, kwamba tangu kuzuka kwa mzozo jimboni TigrayNovemba 2020, vikosi vya usalama vya Amhara pamoja na uongozi wa muda wameendesha kampeni ya takasatakasa ya kikabila dhidi ya jamii ya wa Tigray magharibi mwa Tigray, wakitenda uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Utafiti wa karibuni wa shirika hilo umegundua kuwa maafisa wawili, Kanali Demeke Zewdu na Belay Ayalew, waliolaumiwa huko nyuma kwa kutenda dhulma, wanaendelea kuhusika katika ukamataji wa holela, mateso, na uhamishaji wa lazima wa Watigray.

Naibu mkurugenzi wa Afrika wa Human Rights Watch Laetitia Bader, amesema mapatano ya Novemba ya Ethiopia Kaskazini hayajafikisha mwisho madhila kwa jamii ya Watigranya katika zoni ya magharibi ya Tigray, na kuitaka serikali ya Ethiopia kucha kuzuwia uchunguzi huru juu ya ukatili uliofanywa huko, kuwawajibisha makamanda na maafisa waiohusika, ikiwa kweli inataka kuhakikisha haki inatendeka.

Äthiopien Mekelle | Tigray-Streitkräfte  Übergabe von  Waffen an äthiopische Armee
Vikosi vya Tigray vilianza kusalimisha silaha zao nyepesi na za kati kwa vikosi vya jeshi la shirikisho la Ethiopia Tarehe 26.05.2023.Picha: Million Hailessilasie/DW

Soma pia: Ethiopia imemchagua afisa wa TPLF kuwa rais wa mpito Tigray

Kuanzia Septemba 2022 hadi Aprili 2023, Huma Rights Watch inasema iliwahoji watu 35 kwa njia ya simu, wakiwemo mashahidi na wahanga wa ukiukaji pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo. Wengi wa waliohojiwa ni Watigrinya na walikuwa wamezuwiliwa kiholela katika mji wa Humera.

Waliohojiwa walisema maafisa na vikosi vya Amhara waliwashikilia vizuwizini maelfu ya Watigrinya, katika miji ya magharibi mwa Tigray ya Humera, Rayan na Adebai kwa msingi wa utambulisho wao kabla ya kuwafukuza kwa lazima Novemba 2022 au Januari 2023.

Serikali yasita kuwachukulia hatua watuhumiwa

Mnamo mwezi huu wa Mei, Human Rights Watch iliwasilisha muhtasari wa ugunduzi wake wa awali kwa serikali ya Ethiopia lakini haikupokea majibu. Kufikia Machi, ripoti hiyo inasema wapiganaji katika eneo la Tigray Magharibi waliendelea kuwatishia na kuwanyanyasa Watigrinya.

Watu wengi waliokoseshwa makazi waliiambia Human Rights Watch kwamba wanatumai kurejea nyumbani lakini hawakujisikia salaama kufanya hivyo wakati maafisa waliowatesa na vikosi vya usalama vinaendelea kuwepo.

Chama cha TPLF chawakabili wanajeshi wa Ethiopia Tigray

Soma pia: TPLF yaondolewa katika orodha ya makundi ya kigaidi Ethiopia

Kufikia Oktoba 2022, shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa lilikuwa limesajili wakimbizi wa Ethiopia 47,000 mashariki mwa Sudan, wengi wao wakiripotiwa kukimbia kutoka Tigray Magharibi.

Watigrinya waliohojiwa wameelezea haja ya haki na uwajibikaji, "kuanzia kwa maafisa wa ngazi ya juu hadi wale wa mashinani, raia wa kawaida walioshiriki katika shughuli za uhalifu, wote wahojiwe na kusisitiza haja ya kuwepo na uwajibikaji.

Hata hivyo serikali ya Ethiopia haijaonyesha shauku ya kuwafikisha wahusika wa ukiukaji wa Tigray mbele ya vyombo vya sheria.

Chanzo: HRW